TSH BIL 258.48 KWENYE AFYA MSINGI
ARUSHA
Katika mwaka 2023/24 serikali iliidhinisha shilingi bilioni 258.48 kupitia ruzuku ya serikali kuu, mapato ya ndani na washirika wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za afya ya msingi, ustawi wa jamii na lishe.
Aidha hadi Machi, 2024 shilingi bilioni 253.67 zimepokelewa sawa na asilimia 98.14 ya fedha iliyoidhinishwa.
Shughuli zilizotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa majengo ya hospitali 45 za halmashauri zilizoanza ujenzi mwaka 2020/21 ambapo kila halmashauri iliidhinishiwa fedha kulingana na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Kati ya miradi hiyo, hospitali nne (4) zipo hatua ya umaliziaji, hospitali nne (4) zipo hatua ya kupandisha kuta, hospitali moja (1) ipo hatua ya jamvi na hospitali 36 zipo katika hatua za awali za ujenzi.
