BUREAU DE CHANGE ZILIZOFUNGWA, KUFUNGULIWA

 

BUREAU DE CHANGE ZILIZOFUNGWA, KUFUNGULIWA

BUREAU DE CHANGE ZILIZOFUNGWA, KUFUNGULIWA

DODOMA
Serikali ipo mbioni kufungulia maduka ya kubadilisha fedha nchini (Bureau de change), ambayo yalifungiwa mwaka 2016 kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha
Chanzo:- wizara ya fedha.
Serikali itayafungulia maduka hayo muda wowote kuanzia sasa na kurudishiwa mali na fedha  zote zilizopokwa  katika operesheni iliyofanyika mwaka 2019 kwakuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan haipo tayari kuona rasilimali na fedha za mtu yeyote zilizochukuliwa zimebaki serikalini.
Aidha serikali ilichukua uamuzi wa kufungia maduka hayo ya kubadilisha fedha mwaka 2016, baada ya Benki Kuu ya Tanzania  kufanya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na kugundua miamala mbalimbali kwa baadhi ya maduka, kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za usimamizi wa maduka ya fedha za kigeni.
Pia BoT ilifanya udhibiti  wa utakasishaji wa fedha haramu. Kufuatia hali hiyo, mwaka 2018 na 2019, BoT kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali ilifanya operesheni ya ukaguzi maalum kwenye maduka yote ya kubadilisha fedha za kigeni nchini na kubaini makosa mbalimbali,  ikiwemo kutofanya utambuzi wa wateja kabla ya kutoa huduma kinyume na kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Udhibiti wa Utakatishaji Fedha Haramu, Sura 423 na kanuni ya 17 ya Kanuni za Udhibiti wa Utakatishaji Fedha Haramu
MUHIMU:-  Jumla ya maduka  68 yalifungiwa aidha hadi sasa tayari maduka 61 yameshafunguliwa, huku saba yaliyosalia yakitarajiwa kufunguliwa  muda wowote kuanzia sasa.