TSH BIL 50 KUKARABATI MADARAJA YALIYOKATIKA

 

TSH BIL 50 KUKARABATI MADARAJA YALIYOKATIKA

TSH BIL 50 KUKARABATI MADARAJA YALIYOKATIKA

DODOMA
Serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itajikita katika kufanya matengenezo makubwa katika madaraja yote yaliyokatika na kuhakikisha yanarejeshwa katika hali yake, maeneo korofi yaliyoathiriwa na mvua pamoja na kuendelea kukamilisha utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja hususan ya kimkakati na ile ya kupunguza msongamano katika miji ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es Salaam na Morogoro. 
Ili kufanikisha mpango huu Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 50 ambazo ni fedha za dharura kwa ajili ya matengenezo ya barabara zitakazosaidia kuboresha na kukarabati maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua