TSH BIL 22.3 ZAJENGA MAKAO MAKUU TAKUKURU
DODOMA
Serikali ya wamu ya sita imetoa kiasi cha shilingi bilioni 22.3 kwa ajili ya ujenzi wa makuu makuu ya taaisis ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma, ikiwa ni hatua ya serikali kuboresha miundombinu ya ofisi mbalimbali nchini.
Katika hatua nyingine kwa kipindi cha uongozi wa Mhe Rais Samia jumla ya wafanyakazi 380 wameajiriwa kutokana na Dkt Samia kutoa kibali cha ajira hizo lengo likiwa ni kuongeza rasilimali watu na kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi.
Aidha Mhe Rais ametoa fedha kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya weledi na jumla ya watumishi 1365 wamepata mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
