TSH BIL 4 KUPANUA BARABARA YA NJIA 4 BUKOBA MJINI
KAGERA
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeridhia kuongeza kiasi cha Shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kukamilisha upanuzi wa barabara ya njia nne Bukoba Mjini (Rwamishenye Round about - Stendi ya Bukoba Mjini) yenye urefu kilometa 1.6
Awali Serikali ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.64 kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi eneo la Mitaga ambapo kwa sasa utekelezaji wake umefikia 25%