DAR,BEIJING KUKUZA BIASHARA
DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanzania ina matumaini ya kuongeza zaidi kiwango cha biashara na China kutoka takribani shilingi trilioni 23 hadi trilioni 51 ifikapo mwaka 2030,hii ni kutokana na mageuzi yanayoendelea ya udhibiti ili kuboresha mazingira ya biashara na uboreshaji wa miundombinu ya usafiri na nishati ambayo yatachochea uzalishaji na kuongeza uwekezaji na biashara.
Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDIs) unatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 563.9 za sasa hadi shilingi trilioni 1.3 ndani ya miaka sita ijayo.
Chanzo:- Ofisi ya makamu wa Rais wakati wa kufunga Kongamano la Jukwaa la Uwekezaji kati ya China na Tanzania na Kongamano la Kukuza Biashara na Uwekezaji la China (Jinhua) lililofanyika jijini Dar es Salaam
Aidha China imekuwa mwekezaji mkuu wa kimkakati na mshirika mkuu wa biashara wa Tanzania, kutokana na mtiririko wa fedha wa kila mwaka wa FDI kutoka China (milioni 234.7 mwaka 2019 hadi shilingi bilioni 563.9 mwaka 2021