TSH BIL 33+ ZINALIPIA ELIMU BILA ADA KWA MWEZI

 

TSH BIL 33+ ZINALIPIA ELIMU BILA ADA KWA MWEZI

TSH BIL 33+ ZINALIPIA ELIMU BILA ADA KWA MWEZI

TANZANIA
Jumla ya shilingi bilioni 33.30 zinatolewa na serikali ya awamu ya sita kila mwezi kwa ajili ya ruzuku ya elimu bila ada kutoka shilingi bilioni 13.46 iliyokuwa ikitolewa tangu kuanza kwa mpango huu mwaka 2015/16 ongezeko sawa na 147.26%
Serikali imejidhatiti kutekeleza maelekezo ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa kuendeleza utoaji wa Elimu Bila Ada ili kuhakikisha wanafunzi wote wenye umri wa kwenda shule wanaenda. 
Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kutambua hilo, hadi kufikia machi, 2024 imetoa shilingi trioni 2.31 ili kutekeleza mpango wa Elimumsingi Bila Ada ikiwa ni ruzuku tangu kuanza utekelezaji wa mpango huo Disemba, 2015. 
KATI YA FEDHA HIZO SHILINGI BILIONI 758.81 ZIMETOLEWA KATIKA KIPINDI CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.