MIUNDOMBINU YA MAJI YABORESHWA TEMEKE
TEMEKE
Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam inafanya maboresho ya miundombinu ya maji katika eneo la TCC Sigara kwa kubadilisha miundombinu chakavu katika laini ya inchi 6 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji ili kuboresha huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
