RAIS SAMIA ATOA KIBALI CHA KUAJIRI WATUMISHI 46,000
DODOMA
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 46,000, wa kada tofauti, hii ni kwa mujibu wa wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Kati ya nafasi 46,000 za ajira, ajira 12,000 zitakuwa za walimu, huku nafasi 10,000 zikiwa za watumishi katika sekta ya afya na nafasi zilizosalia zitatolewa kwa kada zingine ambapo nafasi hizo mpya zikishajazwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu kada ya ualimu na watumishi wa umma katika sekta ya afya na nyinginezo
Aidha serikali inafikiria kubuni mbinu mpya ya kuajiri ambapo mamlaka za mikoa zitahusika badala ya kufanya hivyo kupitia kituo kikuu cha uajiri.
