DKT SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI
UTURUKI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo April 18, 2024 ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka chuo kikuu cha Ankara nchini Uturuki kama utambuzi wa jitihada zake za kuendeleza mageuzi ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.
Mh. Dkt Samia amekabidhiwa Shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo ,pia Mhe Rais Samia amepata nafasi ya kuhutubia wageni, viongozi na wananfunzi wa chuo kikuu cha Ankara.
#BimkubwaUturuki
