MISENYI – BUKOBA VIJIJINI KUUNGANISHWA KWA LAMI

 

MISENYI – BUKOBA VIJIJINI KUUNGANISHWA KWA LAMI

MISENYI – BUKOBA VIJIJINI KUUNGANISHWA KWA LAMI

KAGERA
Serikali imepanga kuziunganisha Wilaya za Misenyi na Bukoba Vijijini kwa kuanza ujenzi wa barabara ya Kyaka - Katoro - Kanazi hadi Kyetema yenye urefu wa kilometa 60.7 kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji ndani ya Mkoa wa Kagera
Chanzo:- Wizara yan ujenzi,kupitia mazungumzo na wananchi wa kata ya Katoro na Ibwera katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoani Kagera.
Kuelekea utekelezaji wa mradi huu tayari Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa awamu kwa kuanza na kilometa 10 kuanzia Kanazi hadi Kalonge pamoja na ujenzi wa daraja kubwa la Kalebe