TSH BIL 22 KUBORESHA BANDARI YA B/MOYO
PWANI
Serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025, imetenga jumla ya shilingi bilioni 22 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Kuelekea mchakato huo Serikali imekamilisha kuwalipa fidia wamiliki wa ardhi waliolazimika kuhama ili kupisha utekelezaji wa mradi huo
Mchakato wa uboreshaji wa taarifa unatarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha (2023/2024) na baada ya hapo mchakato wa manunuzi ya mkandarasi kutekeleza mradi utaanza.
Utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa awamu, kulingana na ongezeko la mizigo inayohudumiwa na kituo cha baharini.
Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa gati tatu zenye urefu wa mita 1000 na kina cha mita 15.5.
Aidha utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni moja ya uwekezaji unaolenga kukuza uchumi wa nchi na kuboresha uhusiano wa kibiashara wa kikanda.
