BAJETI YA BARABARA RUKWA YAPAA HADI TSH BIL12.3

 

BAJETI YA BARABARA RUKWA  YAPAA HADI TSH BIL12.3

BAJETI YA BARABARA RUKWA  YAPAA HADI TSH BIL12.3

RUKWA 
Serikali ya Awamu ya Sita  imeongeza bajeti ya barabara  mkoa wa Rukwa kutoka shilingi bilioni 5.63 hadi shilingi bilioni 12.3, Lengo likiwa ni kuimarisha mtandao wa barabara katika mkoa huo.
Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara, vivuko na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani Rukwa ili kuinua shughuli za kijamii na kiuchumi.
Aidha kutoka na ongezeko la bajeti iliyotolewa na serikali, Barabara kiwango cha changarawe zimeongezeka kutoka Km 867.25 hadi Km 1,143.05,pia imefanya marekebisho  mtandao wa barabara za lami na maeneo korofi jumla ya Km 196.66