TARURA- 2025/2026 BARABARA ZITAPITIKA KIPINDI CHOTE
MOROGORO
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeweka mipango mkakati ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025/2026, asilimia 85 ya mtandao wa barabara unapitika kwa misimu yote.
Chanzo:- Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, hivi karibuni, mjini Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa TARURA, cha kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, kitakachowasilishwa na na wizara ya ujenzi kwenye Bunge mwezi ujao.
Lengo kuu la mkakati huo ni kuhakikisha barabara zinaendelea kupitika katika misimu yote ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi.
Hadi sasa ni asilimia 44 pekee ya barabara za TARURA hazijawa na mtandao mzuri, zikiwemo kilomita 3,200 za barabara za lami na zaidi ya kilomita 41,000 za barabara za changarawe ambazo hadi 2025/2026zitakuwa zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Aidha serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuunganisha mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka eneo la wilaya moja hadi nyingine ili kuongeza uharakishaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi na kuongeza kasi ya ongezeko la uchumi