TANZANIA YAJIUNGA NA SOKO LA USAFIRI WA ANGA AFRIKA

 

TANZANIA YAJIUNGA NA SOKO LA USAFIRI WA ANGA AFRIKA

TANZANIA YAJIUNGA NA SOKO LA USAFIRI WA ANGA AFRIKA

DAR ES SALAAM
TANZANIA imezindua mpango wa kujiunga na Soko la Usafiri wa Anga la Afrika (SAATM) ambalo linatoa fursa kubwa za biashara ya usafiri wa anga lengo likiwa ni kuisaidia nchi kuongeza kipato.
Chanzo:- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari ,jijini Dar es Salaam akizungumza wakati wa warsha ya uhamasishaji.
"Kama nchi, tulikuwa nje ya aina hii ya biashara makusudi ili kuongeza na kuimarisha uwekezaji katika mashirika yetu ya ndege, Sasa tunaona kuwa ni wakati mwafaka,” amesema Johari.
Mkutano huo wa siku tatu wa uhamasishaji umejadili masuala makuu mawili ambayo ni uwezekano wa nchi kuingia katika soko moja la usafiri wa anga na uundaji wa marekebisho na utekelezaji wa kanuni mpya za usafiri wa anga. 
Hadi sasa, nchi 34 zimetia saini mkataba wa SAATM zikiwemo Benin, Botswana, Burkina Faso, Cabo Verde, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo Brazzaville, Côte d'Ivoire, Misri, Ethiopia, Equatorial Guinea, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea. (Bissau), Guinea, na Kenya. Nyingine ni Lesotho, Liberia, Mali, Morocco, Msumbiji, Namibia, Niger, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Afrika Kusini, Swaziland, Chad, Togo na Zimbabwe.
Aidha chini ya mwamvuli huu, mashirika ya ndege ya Tanzania yatapata fursa ya kufanya biashara ya abiria na mizigo ndani ya bara zima la Afrika bila vikwazo.
KUMBUKA:- TCAA inasimamia sekta hiyo kwa kanuni, kuziendeleza mara kwa mara ambalo ni jambo muhimu ili kukidhi mahitaji ya soko.