SERIKALI KUJENGA MAKUMBUSHO YA MUUNGANO

 

SERIKALI KUJENGA MAKUMBUSHO YA MUUNGANO

SERIKALI KUJENGA MAKUMBUSHO YA MUUNGANO

DODOMA
Serikali imetangaza kujenga makumbusho kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za Muungano katika mwaka wa fedha 2024/25.
Jumla ya shilingi bilioni  45 zimewasilishwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo 
Hadi sasa serikali zote mbili za Muungano na Zanzibar tayari zimetatua kero 21 za Muungano huku zikiwa zimebakia mambo manne pekee ambayo inakamilisha taratibu za kutatua masuala manne yaliyokuwa yamesalia.
Aidha katika miaka 60 ya Muungano imesaidia uboreshaji wa uchumi, maendeleo katika utoaji wa huduma za kijamii kama vile elimu, maji na afya, uboreshaji wa ulinzi na usalama, utekelezaji wa programu za maendeleo kwa sehemu mbili za Muungano.
Serikali pia imeendelea kutatua changamoto za Muungano, kuboresha ushirikiano katika mambo yasiyo ya Muungano pamoja na kutoa elimu kwa wingi kuhusu mambo ya Muungano