M-MAMA YAWAFIKIA WANANCHI 21,800
TANZANIA
Mpango wa mfumo wa huduma ya usafiri wa dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 06 Aprili, 2022 hadi sasa umewafikia akina mama wajawazito na watoto wachanga 21,800 katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Mpango huu umesaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito vinavyotokana na ukosefu au kuchelewa kupata huduma ya usafiri wa dharura na hadi Oktoba 2023 umeanza kutumika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar