RAIS SAMIA KUZINDUA KITABU CHA MUUNGANO
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua kitabu cha miaka 60 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar leo April 24,2024 Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Kitabu cha miaka 60 ya Muungano kitakuwa ni zana ya mafunzo na elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya Muungano.
Aidha mafanikio muhimu katika miaka 60 ya Muungano, ni pamoja na kudumisha amani, umoja wa kitaifa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi