MIKOPO YA 10% KUTUMIA WEZESHA PORTAL
TANZANIA
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesanifu na kujenga Mfumo wa Wezesha Portal utakaotumika kukopesha mikopo ya asilimia 10.
Matumizi ya mfumo huu yatasaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwa ni pamoja na kuondoa vikundi hewa, watu kujisajili zaidi ya kikundi kimoja, wakopaji hewa, kuimarisha usimamizi, usajili wa vikundi, utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo na upatikanaji wa taarifa sahihi za mikopo kwa wakati ili kuongeza tija, kuondoa upendeleo na kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Benki Kuu ya Tanzania kwa kutambua dhima na walengwa imesanifu na kujenga moduli mbili katika mfumo wa Wezesha Portal kwa ajili ya usajili na usimamizi wa vikundi vya huduma ndogo za fedha (Community Microfinance Groups) pamoja na wahamasishaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha (Business Microfinance Promoters).