MAKUSANYO YAONGEZEKA HADI TSH BIL 848.14

 

MAKUSANYO YAONGEZEKA HADI TSH BIL 848.14

MAKUSANYO YAONGEZEKA HADI TSH BIL 848.14

TANZANIA
Makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi bilioni 625.32 Machi, 2023 hadi shilingi bilioni 848.14 Machi, 2024 ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 222.82
Aidha hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye mamlaka za serikali za mitaa katika kipindi cha Awamu ya Sita imeendelea kuimarika, ambapo makadirio yameendelea kuongezeka kutoka shilingi trilioni 1.01 mwaka 2022/23 hadi shilingi trilioni 1.14 mwaka 2023/24. 
Ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya ndani katika mamlaka za serikali za mitaa, limechangiwa na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali ya awamu ya sita ikiwemo tathmini ya vyanzo vya mapato iliyofanyika kwa miaka miwili (2) mfululizo ya mwaka 2022/23 na mwaka 2023/24 katika halmashauri 184 na matumizi ya mfumo wa TAUSI katika ukusanyaji wa mapato.