MIUNDOMBINU BORA YA ELIMU YAONGEZA UFAULU

 

MIUNDOMBINU BORA  YA ELIMU YAONGEZA UFAULU

MIUNDOMBINU BORA  YA ELIMU YAONGEZA UFAULU

TANZANIA
Kutokana na jitihada zinazofanywa na Mhe Rais Dkt Samia katika kuboresha na kuimarisha mazingira ya kujifunza na kufundishia (miundombinu) ya elimu nchini zimezaa matunda na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita.
katika mwaka wa masomo wa 2023, ufaulu wa kidato cha sita kwa watahiniwa wa shule ulikuwa 99.90% ambapo watahiniwa 96,010 kati ya watahiniwa 96,319 waliofanya mtihani walifaulu. Idadi ya wanafunzi waliofaulu imeongezeka kutoka 84,404 mwaka 2022 hadi 96,010 mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 11,606 sawa na 13.75%