NCAA KUWANIA TUZO VIVUTIO VYA UTALII AFRIKA 2024
ARUSHA
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la NGORONGORO (NCAA) imeteuliwa kuwania Tuzo ya Dunia ya Kusafiri katika kitengo cha Vivutio vya Utalii vinavyoongoza barani Afrika 2024.
Akizungumza mjini Arusha April 28, 2024, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Victoria Shayo, amesema " Kila mmoja wetu anapaswa kuipigia kura Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ikiwa tutashinda shindano hili, tuzo hiyo itasaidia nchi yetu kuleta watalii wengi, kuingiza fedha za kigeni na pia kuboresha uchumi wa nchi," amefafanua.
Kumbuka Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zinazoshiriki kinyang’anyiro cha tuzo hizo, nyingine ni Misri, Malawi, Botswana na Afrika Kusini.
ZINGATIA:-NCAA ilishinda tuzo ya utalii ya dunia mwaka jana(2023) na mwaka huu tukiipigia kura Tanzania itashinda kwa mara mbili mfululizo.
NCAA IKISHINDA, TANZANIA IMESHINDA
