MRADI WA KUZALISHA UMEME (MAJI) RUHUDJI UNAENDELEA.

 

MRADI WA KUZALISHA UMEME  (MAJI)  RUHUDJI UNAENDELEA.

MRADI WA KUZALISHA UMEME  (MAJI)  RUHUDJI UNAENDELEA.

NJOMBE
Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa mto Ruhudji – MW 358  kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. 
Hadi sasa tayari uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi umekamilika na taratibu za kulipa fidia zinaendelea. 
Aidha, vyeti vya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimeshatolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). 
Vilevile, tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi imekamilika na taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu hiyo zinaendelea