MWAKA 202324 KATA 1,137 ZATUMIA MFUMO WA KIHASIBU

 

MWAKA 202324 KATA 1,137 ZATUMIA MFUMO WA KIHASIBU

MWAKA 202324 KATA 1,137 ZATUMIA MFUMO WA KIHASIBU

TANZANIA
Katika mwaka 2023/24 kata 1,137 mitaa na vijiji 5,728 vimeanza kutumia Mfumo wa Kihasibu na Utoaji wa Taarifa za Fedha katika Ngazi za Msingi (FFARS) na kufanya jumla ya vituo 49,883 vinavyotumia FFARS ikiwemo vituo vya kutoa huduma za afya na elimu. 
Matumizi ya mfumo yameleta uwazi, uwajibikaji na udhibiti wa matumizi ya fedha katika ngazi za msingi za mamlaka za serikali za mitaa. 
kupitia mfumo huo, wananchi na wadau wote wanao uwezo wa kupata taarifa za mapato na matumizi ya fedha zote zinazoingia katika maeneo yao.