MW 2,138 ZA UMEME ZAUNGANISHWA GRIDI YA TAIFA

 

MW 2,138 ZA UMEME ZAUNGANISHWA GRIDI YA TAIFA

MW 2,138 ZA UMEME ZAUNGANISHWA GRIDI YA TAIFA

TANZANIA
Katika mwaka 2023/24 Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia Machi, 2024 uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ulifikia jumla ya MW 2,138 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na MW 1,872.1 za Mei, 2023.
Katika kiasi hicho MW 836.3 ( 39.1%) ni umeme unaotokana na nguvu ya maji, MW 1,198.8 (56.1%) gesi asilia, MW 92.4 (asilimia 4.3) mafuta mazito na MW 10.5  (0.5%) na tungamotaka (biomass)
Ongezeko la uwezo wa uzalishaji wa umeme limetokana na kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (MW 2,115) ambapo MW 235 zimeanza kuzalishwa kupitia mtambo Namba 9 pamoja na kukamilika kwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rusumo ambao unachangia MW 26.7 katika Gridi ya Taifa.