MV 49.5 ZINAZALISHWA MALAGARASI
KIGOMA
Jumla ya MW 49.5 zinazalishwa kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi katika Kigoma.
Pamoja na uzalishaji huo pia ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 54 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe, mkoani Kigoma umefanikiwa.
Aidha Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme anaendelea na kazi za ujenzi ambapo utekelezaji umefikia 15.6% na mradi unatarajiwa kukamilika Aprili, 2025
