DKT SAMIA AMPOKEA RAIS WA SOMALIA MHE. MOHAMUD IKULU
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo April 27, 2024 amempokea na kufanya nae mazungumzo Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud aliyekuja nchini kwa ziara ya kitaifa kuanzia leo April 27, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Pamoja na mambo mengine Marais wa nchi hizo mbili wamesimama pamoja wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa, pia wakati wa mapokezi Rais Mohamud amepata nafasi ya kukagua gwaride, kisha kufanya mazungumzo na waandishi wa habari.
