ELIMU MUBASHARA KUFANYA KAZI NCHINI

 

ELIMU MUBASHARA KUFANYA KAZI NCHINI

ELIMU MUBASHARA KUFANYA KAZI NCHINI

TANZANIA
Serikali kupitia OR-TAMISEMI na Shirika la Elimu Kibaha limeandaa Mfumo wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (e-learning management system) kwa ajili ya kutoa elimu ya sekondari mubashara (Live teaching) kwa shule za sekondari ili kuongeza nguvu kwenye ufundishaji wa masomo ya sayansi na hisabati. 
Hadi Machi, 2024 ujenzi wa mfumo umeendelea na majaribio ya kutoa elimu ya sekondari mubashara yamefanyika katika Shule za Sekondari za Kibaha na Dodoma na matarajio ni kuzifikia shule zote za sekondari hususan katika masomo ya sayansi na hisabati.