DKT SAMIA ATOA SALAMU ZA PASAKA

 

DKT SAMIA ATOA SALAMU ZA  PASAKA

DKT SAMIA ATOA SALAMU ZA  PASAKA 

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewatakia heri ya sikukuu ya pasaka waumini wa dini ya kikristo nchini na duniani kote leo 31 Machi wanapoadhimisha kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
Kupitia kurasa zake za mitandoa ya kijamii Mhe Rais Samia ameandika"  Kheri ya Sikukuu ya Pasaka kwenu nyote. Katika siku hii ambayo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, tuendelee kujifunza katika upendo wake mkuu wa kujitoa kwa ajili ya wengine. 
Upendo kwa muumba wetu, utusukume kuishi katika njia iliyo njema. Upendo kwa ndugu, jamaa na jirani zetu, utusukume kuendelea kuliombea Taifa letu amani, umoja na mshikamano. 
Upendo kwa wale tunaotofautiana nao, utusukume kutafuta na kuishi katika maridhiano na ustahimilivu. Upendo kwa nchi yetu, utusukume kuitumikia kwa weledi na kila wakati kukusudia kupiga hatua mbele zaidi kwa kujenga upya" 
Bimkubwatanzania tunaungana na Mhe Rais kuwatakia heri ya sikukuu ya Pasaka.