MIRADI 9 YA MAJI INATEKELEZWA NYANG’HWALE

 

MIRADI 9 YA MAJI INATEKELEZWA NYANG’HWALE

MIRADI 9 YA MAJI INATEKELEZWA NYANG’HWALE 

GEITA
Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 9 katika vijiji vya Iseni, Kabiga, Nyangalamila, Nwiga, Kasubuya, Nyamikonze, Nyijundu, Bululu na Ifugandi vilivyopo katika wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita ambapo kukamilika kwake kutanufaisha wananchi wa vijiji hivyo ikiwa ni pamoja na shule za msingi na sekondari 10 zinazopatikana kwenye vijiji hivyo.
Serikali imekamilisha usanifu katika vijiji vingine katika wilaya hiyo yenye vijiji 62  ili kuhakikisha vinafikiwa na huduma ya maji ikiwa ni pamoja na shule za msingi na sekondari zilizopo katika vijiji hivyo aidha,kazi ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji itaanza kufanyika katika mwaka wa fedha 2024/25 ili kuimarisha huduma ya maji katika maeneo hayo.