DKT SAMIA AWATUNUKU NISHANI VIONGOZI
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo April 24, 2024 amewatunuku nishani viongozi mbalimbali wakati wa shamrashamra za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika viwanjan vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Pamoja na wengine Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal