MHE.RAIS DKT SAMIA KUFANYA ZIARA UTURUKI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara nchini Uturuki kuanzia tarehe 17 hadi 21 April 2024 baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Uturuki Mhe. Tayyip Erdogan.
Ziara hii ina lengo la kukuza uhusiano wa kidiplomasia ya siasa, uchumi, na biashara, pia kupata mtaji wa teknolojia ambao nchi ya Uturuki wanayo , kupata masoko ya bidhaa ambayo yapo nchini humo na kupata wawekezaji kwa lengo la kuwekeza nchini Tanzania
