BAJETI YA TARURA PWANI YAONGEZEWA KUTOKA TSH 11 HADI TSH 32
PWANI
Serikali ya Awamu ya Sita imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara za wilaya nchini ambapo imeongeza bajeti ya TARURA mkoa wa Pwani kutoka shilingi Bilioni 11 hadi kufikia shilingi Bilioni 32.
Hadi sasa serikali imeongeza mtandao wa barabara za lami kutoka Km 56 hadi Km 97 katika Mkoa wa Pwani ambao umejielekeza zaidi kwenye shughuli za viwanda kama sehemu ya uchumi na eneo mojawapo ambalo limenufaika ni barabara ya Visiga- Zegereni ambapo zaidi ya Km 12.5 za barabara zimeshakamilika.
Mkoa wa Pwani una mtandao wa barabara jumla ya Km 5,140 kati ya hizo Km 95 ni lami, Km 1,100 ni changarawe na Km 3,945 ni udongo.
