BARABARA ZA MAWE ZAOKOA TSH BIL 25.5
TANZANIA
Kiasi cha shilingi bilioni 25.5 kimeokolewa kwa serikali kujenga barabara zenye urefu wa km 23.18 na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 8.1ambapo ingetumia shilingi bilioni 12.8 kama ingejenga kwa kutumia lami nyepesi (double surface dressing) na bilioni 33.6 kama ingetumika lami ya zege (Asphat Concrete)
Aidha serikali imejenga madaraja makubwa sita ambayo ni Berega 140m Kilosa, Msadya 60m Mpimbwe, Mwasanga 40m Mbeya, ujenzi wa madaraja ya Kiwila 40m Ileje, Mkomanzi 60m Korogwe na Kalambo 80m Kalambo unaendelea kukamilishwa.
MUHIMU:- Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, takribani shilingi Trilioni 2.53 zimepokelewa na TARURA kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini na mijini.
