MADINI YALETA TSH TRIL 1+

 

MADINI YALETA TSH TRIL 1+

MADINI YALETA TSH TRIL 1+

DAR ES SALAAM: 
Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi  wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Madini imekusanya  kiasi cha Shilingi Trilioni 1.9  kutoka katika  vyanzo mbali mbali ikiwemo ada za leseni, ada za ukaguzi za kijiolojia, mrabaha na faini mbali mbali.
-Chanzo:_ wizara ya madini
Mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka  hadi kufikia 9.1% mwaka 2022 na kati ya kipindi cha robo ya tatu Julai hadi  Septemba   mwaka 2023 sekta ilichangia 10.4% ikilinganishwa na mchango wa 9.5% katika kipindi kama hicho mwaka 2022.
-Mwenendo huu wa mchango unaakisi dhamira ya serikali kuhakikisha sekta hiyo inaimarika na kuweza kuchangia hadi asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025
-katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kusimamia biashara ya madini katika masoko ya madini hapa nchi ili kuhakikisha yanafanya kazi kwa ufanisi,  aidha shughuli za uchimbaji na biashara ya madini zimeendelea kuongezeka ambapo jumla ya masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 100 vimeanzishwa nchini