DKT SAMIA AKUTANA NA MKE WA SANJAY DUTT
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo April 06,2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjasiriamali Maanayata Dutt ambaye pia ni mke wa muigizaji nguli wa filamu kutoka India Sanjay Dutt, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Pamoja na mazungumzo yao, Mhe Rais Samia amemkabidhi Bi Maanayata Dutt zawadi ya picha ya mlima Kilimanjaro.