DKT SAMIA AYAGUSA MAISHA YA WASICHANA DINYECHA SEC.

 

DKT SAMIA AYAGUSA MAISHA YA WASICHANA DINYECHA SEC.

DKT SAMIA AYAGUSA MAISHA YA WASICHANA DINYECHA SEC.

MTWARA.
Jumla ya wanafunzi 48 wa shule ya sekondari ya Dinyecha iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba Mkoani Mtwara  (leo) April 20 wamefanya mahafali ya kwanza ya kidato cha  sita (wasichana) baada ya serikali ya awamu ya sita kuipandisha hadhi shule hiyo na kuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa wasichana.
Katika awamu tofauti serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jumla ya shilingi bilioni 1.82  zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni hatua iliyofanikisha wanafunzi hao kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (wasichana) katika shule hiyo ambayo ni ya pekee Mtwara DC inayobeba wanafunzi wa kidato cha 5&6 (wasichana)
Aidha katika kiasi hicho cha fedha serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 560 (awamu ya kwanza) na shilingi milioni 120 (awamu ya pili) huku wadau wengine wa maendeleo wakichangia kiasi cha shilingi bilioni 1.2