KILA MTU ANASTAHIKI KUHESHIMIWA:- DKT SAMIA

 

KILA MTU ANASTAHIKI KUHESHIMIWA- DKT SAMIA

KILA MTU ANASTAHIKI KUHESHIMIWA- DKT SAMIA

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka bayana kulindwa kwa taarifa binafsi za watu au kulindwa kwa haki za binadamu lakini kulindwa kwa miongoni mwa haki za binadamu ni pamoja na kulindwa  kwa haki za faragha.
Dkt Samia amesema hay oleo April 3, 2024 wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya Ukiukwaji wa Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.
Mhe Rais Samia amesema “kwa mujibu wa ibara ya 16 (1) ya katiba ya Jmahuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila mtu anastahiki kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafasi yake na maisha yake binafsi na familia yake, Aidha ibara ya 16(2) ya katiba ilizitaka mamlaka za nchi kuweka utaratibu wa kisheria wa namna ya kulinda haki ya faragha nchini”
Aidha kupitia hotuba hiyo Dkt Samia amesisistiza kuwa ibara ya 12 ya tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 linayataka mataifa kuweka utaratibu unaohakikisha mtu yoyote haingiliwi katika faragha yake,familia,nyumbani au kwenye makazi yake, wala kuvunjiwa heshima, utu au hadhi yake.
Rais  Samia amesema uzinduzi wa tume hiyo ni matakwa ya kikatiba lakini pia ni kutimiza utekelezaji  wa ilani ya chama cha mapinduzi  na kutimiza wajibu wa kikanda  na kimataifa.