BIMKUBWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA MAAFA YA MAFURIKO
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan (leo) April 13, 2024 ameongoza kikao maalum kilichowasilisha ripoti ya maaafa ya Mafuriko yaliyotokea Rufiji Mkoani Pwani,Morogoro, Lindi na Arusha.
Kikao hicho kimefanyika Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar ambapo pamoja na uwaslishaji wa ripoti ya mafuriko,kamati maalum imewasilisha pia maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.