DARAJA LAZIUNGANISHA MINYUGHE NA MAKILAWA, IKUNGI
SINGIDA
Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu
Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mabey Bridge) lenye urefu wa mita 30 kumewezesha mto Minyughe kufunguka na hivyo kutoa fursa kwa shughuli za uchukuzi kuendelea kati ya barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi na litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa vijijini na makao makuu ya mkoa.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia kukamilika kwa kazi hiyo, akiwemo Bi. Elizabeth Bakari wa Kijiji cha Minyughe, na diwani wa Kata Minyughe , Mhe. Nelson Kiwesi, wameishukuru Serikali kwa mradi huo ambao baada ya kukamilika unakwenda kuondoa adha ya usafiri hasa kwa wajawazito
CHUKUA HII:- Daraja hilo la chuma ni la tatu kujengwa hapa nchini, likitanguliwa na mengine yaliyopo Kihansi huko Kilombero na lile la Mbuchi Kibiti, mkoani Pwani.
