WANANCHI 422,446 WAGUSWA NA DKT SAMIA UTOAJI HAKI

 

WANANCHI  422,446 WAGUSWA NA DKT UTOAJI HAKI

WANANCHI  422,446 WAGUSWA NA DKT SAMIA UTOAJI HAKI

DODOMA
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Mhe Rais Dkt Samia amewezesha wananchi 415,280 na wafungwa 7,166 kupata huduma za kisheria bila malipo kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyozinduliwa katika vijiji 1,348 vya mikoa sita nchini.
Huduma ya msaada wa kisheria inayotolewa kupitia kampeni hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupanua uelewa wa wananchi katika masuala ya kisheria na kutatua migogoro mbalimbali na utoaji wa huduma za kisheria katika masuala mbalimbali.
Dhamira ya Dkt Samia ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa watu wote bila kujali hali zao za kiuchumi,kampeni hii  imewezesha kuimarika kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika utoaji wa huduma za mahakama na kuandika nyaraka za kisheria, huku serikali ikikamilisha tafsiri ya awali ya sheria 258.
Aidha katika kutekeleza maono ya Dkt Samia ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati, Serikali imeanzisha Kituo cha Mawasiliano cha Huduma kwa Wateja kwa ajili ya kupokea malalamiko, maombi ya huduma za kisheria, taarifa na maoni ( Mawasiliano Centre) kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa masuala ya haki.
Pia Ili kuharakisha usikilizaji na umalizaji wa mashauri katika ngazi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, jumla ya majaji 61 wameteuliwa kati ya Machi 2021 na Februari 2024 kati yao majaji 19 ni wa Mahakama ya Rufani na 42 wa Mahakama Kuu.
Kwa Mantiki hii,  hadi kufikia Februari 2024, kulikuwa na jumla ya majaji 135, kati yao 100 wanatumikia Mahakama Kuu na 35 katika Mahakama ya Rufani, ikilinganishwa na majaji 74, kati yao 58 walikuwa wa Mahakama Kuu na 16 katika Mahakama ya Rufani. 
Pia Serikali imefanya maboresho ya mifumo ya TEHAMA ya Huduma za Mahakama ambayo imewezesha kurahisisha usajili na upangaji wa mashauri kwa njia ya mtandao, upatikanaji wa wakati wa maendeleo ya kesi na nakala za hukumu, kupunguza gharama za usikilizwaji wa mahakama na wadau na kurahisisha tafsiri ya hukumu na kumbukumbu za kesi.