SERIKALI KUIPA NGUVU SEKTA YA MUHOGO

 

SERIKALI KUIPA NGUVU SEKTA YA  MUHOGO

SERIKALI KUIPA NGUVU SEKTA YA  MUHOGO

DODOMA
SERIKALI imesema itaendelea kutengeneza fursa katika sekta ya zao la muhogo hasa katika kutafuta masoko.
Uhakika huo umetolewa na wizara ya kilimo Bungeni  mjini Dodoma  na kusema kwamba serikali inatekeleza mipango mbalimbali ya kuvutia wateja wa zao hilo kutoka duniani kote, ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya uhakika pamoja na kuandaa vikao vinavyohusu biashara ya muhogo.
“Katika kutekeleza hilo, wizara inaendelea na maandalizi ya ujenzi wa soko kubwa la muhogo wilayani Kahama pamoja na miundombinu ya kukaushia muhogo mkoani Kigoma katika jitihada za kuendeleza bidhaa hiyo’’ imesema taarifa ya wizara
Kwa mujibu wa wizara hiyo, serikali ilikuwa ikiimarisha kwa usawa kampeni katika mnyororo wa thamani wa biashara ya zao la muhogo ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wakulima na wafanyabiashara kujiunga na Chama cha Wazalishaji na Wasindikaji wa Muhogo Tanzania (TACAPPA).
TACAPPA inalenga kuwaunganisha wahusika katika mnyororo wa thamani wa zao la muhogo nchini Tanzania na ni chombo mwamvuli cha kushughulikia masuala yanayowakabili wazalishaji na wasindikaji wa zao hilo nchini ambayo inawajibika kwa kuandaa mipango ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora za muhogo kwa wakulima pamoja na kukuza uelewa juu ya changamoto zinazokabili uzalishaji wa muhogo na jinsi ya kuzitatua