TANZANIA KITOVU CHA UCHENJUAJI AFRIKA
SAUDI ARABIA
Tanzania imedhamiria kuwa kitovu cha uchenjuaji na uongezeaji thamani madini kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati,Lengo likiwa ni kuongeza fursa za ajira na mapato kutokana na mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini.
Chanzo:- Wizara ya madini Jijini Riyadh, Saud Arabia kwenye mkutano mkubwa wa madini uliojadili nafasi ya madini katika maendeleo ya nchi wazalishaji wa madini.
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa kusimamia uongezaji thamani madini kwa kuendelea kuchukua hatua za kupitia mapitio ya sera na sheria juu ya kuweka msisitizo kwenye uongezwaji wa thamani ya madini yanayozalishwa nchini ili kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kunufaika kupitia mnyororo wa thamani wa madini.
Mradi wa Kabanga Nickel-Ngara, mkoani Kagera unaomilikiwa kwa ubia kati ya serikali na wabia ni mfano wa mkakati wa serikali katika kuhamasisha uongezaji thamani nchini Tanzania,kwa kuwa kutajengwa mradi wa kisasa wa kusafisha madini (Multi-metals facility) ya nickel na madini mengineyo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambao utatumia Teknolojia ya kisasa ya Hydromet ili kutosafirisha madini hayo yakiwa ghafi na hivyo kusaidia nchi kupata mapato zaidi,ajira kuongezeka na kukua kwa teknolojia kutokana na usafishaji huo.
Mkakati wa sasa wa Tanzania kupitia sera na sheria za madini ni kuona madini hayo yanaongezwa thamani nchini,hii itaifanya Tanzania kuwa kati ya maeneo machache barani Afrika yatakayosimamia uongezwaji thamani wa madini mkakati.
