MRABAHA, ADA YA UKAGUZI MADINI ZAINGIZA TSH BIL 476.78.
DAR ES SLAAM
Jumla ya shilingi bilioni 476.78 zimechangia makusanyo kutoka kwenye mrabaha na ada ya ukaguzi wa mauzo ya madini katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024
Madini yaliyouzwa ni kiasi cha tani 52.9 za madini ya dhahabu, tani 1,204.83 za madini ya Bati, karati 54,025.89 za madini ya Almasi,karati 183,551.87 na tani 121.34 za madini ya tanzanite na kiasi cha karati 171,286.92 na tani 94,647.94 za madini mengine ya vito yaliuzwa katika masoko ya madini.
