WALIOPISHA UJENZI (EACOP) WAJENGEWA NYUMBA 339

 

WALIOPISHA UJENZI (EACOP) WAJENGEWA NYUMBA 339

WALIOPISHA UJENZI (EACOP) WAJENGEWA NYUMBA 339 

TANGA
Jumla ya nyumba 339 zimejengwa kwa ajili ya makazi ya kudumu kwa wanufaika waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi nchini.
Mkoa wa Tanga pekee mradi umejenga nyumba za makazi mbadala 43 kwa ajili ya wananchi 40 waliopoteza makazi kwenye maeneo mbalimbali ya mkuza ambayo yanapitiwa na mradi huo mkoa huo.
Mratibu wa bomba la mafuta upande wa Tanzania, Asiad Mrutu amesema kuwa jumla ya walioguswa na mradi 9,822 kati ya 9,904 wamelipwa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 34.9 mpaka Sasa.
MUHIMU:-Mradi huo umezingatia sheria za nchi na taratibu za kimataifa katika ulipaji wa fidia ikiwemo kutwaa ardhi