WAKENYA WATUA NCHINI KUJIFUNZA UBORESHAJI SEKTA YA AFYA

 

WAKENYA WATUA NCHINI KUJIFUNZA UBORESHAJI SEKTA YA AFYA

WAKENYA WATUA NCHINI KUJIFUNZA UBORESHAJI SEKTA YA AFYA 

DAR ES SALAAM
Mageuzi makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya Afya nchini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yameivutia Jimbo la Kilifi kutoka nchini Kenya ambao wamefika kujifunza namna Tanzania ilivyofikia hatua hiyo.
Hayo yamesemwa na  mbunge wa Jimbo la Kilifi na Waziri wa Afya Nchini Kenya Mhe. Peter Samwel Mwarogo akiwa na Wabunge wa Kamati ya Afya ya Jimbo hilo ambao hivi karibuni wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kuona mageuzi kupitia huduma, uwekezaji vifaa tiba, uboreshaji miundombinu na utawala.
"Tumekuwa tukisikia maboresho ya huduma Tanzania hususani Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo tumekuja kujifunza mambo mengi mtambuka ili tukaboreshe sekta ya Afya kwa ujumla wake katika Jimbo letu" amesema Mhe.Mwarogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Afya wa Jimbo hilo (Kilifi) Mhe. Edward Zero, amesema wameona mambo mengi ambayo ni chachu kwao kwenda kuyafanyia kazi.
Pamoja na hayo wamejadiliana na Menejimenti ya Hospitali kuhusu usimamizi wa Hospitali, kusomesha watalaam, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, malipo ya huduma kwa makundi mbalimbali.
Aidha, wameelezwa kuhusu uendeshaji wa mtambo wa kuchoma taka, uendeshaji Kliniki za wagonjwa wa kulipia, uwajibikaji wa watumishi, uendeshaji Idara ya dharura, radiolojia na masuala mengine mengi.