TSH BIL 70.5 KUTOA MAJI YA ZIWA VICTORIA HADI BUTIAMA

 

TSH BIL 70.5 KUTOA MAJI YA ZIWA VICTORIA HADI BUTIAMA

TSH BIL 70.5 KUTOA MAJI YA ZIWA VICTORIA HADI BUTIAMA

MARA
Serikali ya awamu ya sita katika mbio za kutekeleza mpango wa kumtua mama ndoo kichwani, Imetoa kiasi cha shilingi bilioni 70.5 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama ambao umetoa maji ziwa victoria hadi wilaya hiyo ya Butiama Mkoani Mara na utekelezaji wa mradi huu umefikia 97%
Kukamilika kwa mradi huu mkubwa kutawaondolea changamoto wananchi wa Butiama ambao kwa sasa wanatumia maji ya mradi wa muda mrefu ambao unazalisha maji yasiyo toshelevu, hivyo mradi huo utamaliza changamoto ya uhaba wa maji katika mji wa Butiama.