VIONGOZI WA KIMATAIFA WANENA, KIFO CHA ALHAJ MWINYI
ZANZIBAR
Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wameungana na Watanzania kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaawamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakisema kwamba urithi wa marehemu utaendelea kuwa msukumo kwa viongozi wa Afrika na duniani kwa ujumla.
Akihutubia umati wa watu waliojitokeza katika Uwanja wa New Amaan Sports Complex mjini Zanzibar Jumamosi kwa ajili ya mazishi ya kitaifa, Makamu wa Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah amesema kuwa marehemu Mwinyi amefuata vyema nyayo za muasisi wa Taifa hilo Mwalimu Nyerere na kama nchi wamefaidika na michango yake mbalimbali.
“Mwinyi alikuwa mmoja wa viongozi wa Afrika ambao wametoa mchango mkubwa katika kurekebisha majumuisho ya ushirikiano kati ya wananchi wa Tanzania na watu wa dunia kwa kufuata nyayo za Mwalimu Julius Nyerere na Namibia ni miongoni mwa nchi nyingi ambazo zimenufaika kwa kiasi kikubwa katika uimarishaji wa saruji, mahusiano ambayo yanaendelea kukua”
Mhe Netumbo Nandi-Ndaitwah ameongeza kwa kusema “Nchini kwetu kuna msemo unasema kuwa msikie rafiki yako anaposherehekea lakini si anapokuwa anaomboleza lazima uende. Tunatoa pole kwa watu wa Tanzania na familia ya Ali Hassan Mwinyi”.
Nae Spika wa Bunge la Burundi, Emmanuel Sinzohagera amesema kifo cha shujaa huyo si hasara kwa Watanzania pekee bali kwa Afrika na dunia nzima.
"Tunapoomboleza kiongozi aliyeaga, tunaomba kwamba urithi wake uendelee kutia moyo vizazi vya sasa na vijavyo. Mzee Mwinyi aliiweka Tanzania katika anga za kimataifa kupitia busara zake na uongozi uliotiwa moyo. Atakumbukwa sana…ni hasara kubwa si kwa Tanzania pekee bali kanda, Afrika na dunia nzima,” Spika wa Bunge la Burundi, Emmanuel Sinzohagera ametoa maoni yake.
#PumzikaKwaAmaniMzeeMwinyi.
