"MAKTABA YETU ILIYOSHEHENI VIZURI IMETEKETEZWA"- DKT SAMIA

 

MAKTABA YETU ILIYOSHEHENI VIZURI IMETEKETEZWA- DKT SAMIA

MAKTABA YETU ILIYOSHEHENI VIZURI IMETEKETEZWA- DKT SAMIA

ZANZIBAR
Rais wa Jmahuri a Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekitaja kifo cha Ali Hassan Mwinyi kuwa ni sawa na maktaba yenye shehena iliyochomwa moto.
Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa shujaa huyo katika viwanja vya New Amaan Sports Complex mjini Zanzibar Jumamosi, Dkt Samia amesema kuwa marehemu Mwinyi alifanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi, jani linalopaswa kuazimwa na viongozi wa umma.
"Nakumbuka mithali ya Kiafrika isemayo 'mzee anapokufa, maktaba huchomwa' ikimaanisha kuwa chochote ambacho mzee anacho, anapokufa, ni kama maktaba iliyochomwa kwani kila kitu kimepotea," Rais Samia amewaambia umati wa watu waliohudhuria hafla hiyo.
“Mtakubaliana nami kuwa Maktaba yetu iliyosheheni vitu vizuri imeteketezwa, alikuwa Maktaba inayotembea ambayo ilikuwa na vitabu vya uaminifu, mabadiliko ya kiuchumi, ujasiri, unyenyekevu na hofu ya Mungu,” amesema.
Pia, Mhe Rais Samia ameeeleza kuwa kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa marehemu Mwinyi kwani ndiye mtu wa kwanza kuwa Rais wa Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Pamoja na kukabiliwa na matatizo ya kisiasa na kiuchumi, marehemu Mwinyi alirekebisha hali iliyopelekea ukuaji wa uchumi Zanzibar na Tanzania Bara,Chini ya uongozi wake, nchi ilishuhudia mageuzi muhimu ya kijamii na kiuchumi na kisiasa ambayo yanafungua njia ya ukombozi wa soko na biashara huria”
#PumzikaKwaAmaniMzeeMwinyi.