USIPITWE- BAJETI NIRC YAFIKIA BIL 373.5
DODOMA
Katika kuhakikisha wizara ya kilimo inachangia pato la Taifa kwa asilimia 10, serikali ya awamu ya sita imeongeza bajeti kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kufikia shilingi bilioni 373.5 kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 kutoka shilingi bilioni 46.5 kwa mwaka 2021/2022.
Hatua ya ongezeko la bajeti hiyo inazingatia mahitaji halisi ya Tume hiyo na Wizara ya Fedha kuongeza ukomo wa bajeti ya Tume hususan bajeti ya Matumizi Mengineyo kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi.
Lengo la serikali ya awamu ya sita kuongeza bajeti katika sekta ya umwagiliaji ni kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza mchango wa umwagiliaji katika pato la Taifa.
